picha

UFUGAJI

SAMAKI
 



Ufugaji Mseto wa Sato na Kambale



Polyculture ni uzalishaji wa samaki aina mbili au zaidi ndani ya mazingira ya maji. Kwa kawaida polyculture hutokea katika mabwawa. Samaki aina ya kambare na sato wanaweza kutumika. Aina hizi za samaki zinafaa na huleta mafanikio mazuri.
Aidha vigezo vya kuchagua samaki kwa ajili  ya polyculture ni hivi hapa chini;

  • Kiwango cha juu ukuaji wa aina ya samaki;
  • Samaki wanaohitajika kwa wingi katika masoko;
  • Chagua aina wale ambayo wana kiwango cha juu cha ukuaji na kiwango cha chini cha vifo katika ukuaji;
  • Aina ambayo hawakupatwi na magonjwa kwa urahisi.samaki ambao ni phytoplankton vorous au omnivorous.

Katika  polyculture, masuala ya kuzingatia ni kama vile Chakula, Mavuno na Masoko yanahitajika kwanza.
Msongamano wa samaki katika bwawa  unaosababishwa na uzalianaji wa Sato (Oreochromis niloticus) ambao husababisha  mashindano katika kula chakula na matokeo yake ni mavuno ya samaki kuwa wadogo sana na thamani yao kushuka chini katika masoko. 
Moja ya mikakati ya kudhibiti kuzaliana kwa wingi kwa sato katika bwawa ni polyculture
Miaka michache iliyopita ,Kambare (Clarias gariepinus), wamechunguzwa na kujulikana kama wana uwezo mkubwa katika polyculture. 
Hata hivyo, idadi ya Sato inaweza kupunguzwa kwa ufugaji mseto wa Sato pamoja na samaki Predator. 










UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI 

Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne (Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini. Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote ulimwenguni.
Lengo la makala haya ni kutoa maelezo ili kusaidia wafugaji wa kiwango kidogo katika nchi
zinazostawi, katika kupunguza umaskini. Sehemu ya kwanza (I) itatoa maelezo kuhusu ufugaji na
hasa ufugaji wa kuku, Sehemu ya pili (II) itaangazia maswala yafuatayo katika kuinua hali ya uchumi
kwa kufuga kuku:
1. Kuendeleza ufugaji wa kuku za kienyeji kwa kutumia njia zisizohitaji gharama nyingi.
2. Kutafuta mbinu na njia muafaka za kuzalisha viwango vya kuku bora kwa njia ya kiasili.
3. Matumizi ya njia za kiasili au zile zisizo gharimu pesa nyingi kutibu na kuzuia magonjwa ya
kuku.

UMUHIMU WA UFUGAJI WA NJIA YA KIENYEJI

Ufugaji wa kuku katika nchi zinazostawi waweza kugawanywa mara mbili: 1) Ufugaji wa
kitamaduni au kienyeji pasipo kuwepo gharama, na 2) Ufugaji wa kisasa unaohitaji fedha nyingi.
Ufugaji wa viwango vikubwa kwa kuzingatia mfumo wa kisasa ni maarufu katika kuzalisha kuku wa
nyama na wale wa mayai. Mfumo huu hujumuisha asilimia ndogo sana ya aina ya ufugaji.
Itafahamika kwamba mfumo wa kisasa haujaadhiri ule wa kienyeji. Idadi kubwa ya watu katika nchi
za hari hutegemea mfumo wa kienyeji kwa nyama na mayai.
Mfumo wa kisasa huhitaji pesa nyingi za kununua vyakula vya kuku. Aidha mfumo wa kisasa huhitaji kazi nyingi ili kutekeleza. Mfumo wa kisasa
umefaulu katika nchi zilizostawi kutokana na hali nzuri ya kiuchumi katika kuzalisha (kuku wa hali
ya juu, kuangua vifaranga kwa stima, vyakula vilivyo na madini mengi, vifaa na zana za mashine,
utaalamu wa hali ya juu n.k). Haitafaa sana kuanzisha mfumo kama huu katika vijiji vya mataifa
yanayostawi.
"Mageuzi" katika ufugaji (kuambatanisha mfumo wa kisasa pamoja na ule wa kienyeji) yamefanyiwa
majaribio katika mataifa yanayostawi tangu miaka ya 1950. Matokeo ya kuku wapatao 200 hadi 300
kwa shamba moja hayajawai kufaulu. Hasara imepatikana na waweza kuona nyumba zilizokuwa na
kuku bila chochote, pesa nyingi zimepotea na kuku hawapo.
Mfumo wa kienyeji ni bora (Katika hali ya kiuchumi) iwapo idadi ya kuku haitazidi kuku 50. Ni
rahisi kuweza kuwatunza kuku, kwani hakuna gharama nyingi. Iwapo vyakula au zana za kisasa
zitanunuliwa, basi haitakuwa kwa viwango vikubwa. Mazao ya nyama na mayai yataleta faida.
Sehemu nyingi katika mataifa yanayostawi hakuna stima, katika nchi za hari, ufugaji kwa kiwango
kidogo umeweza kufaulu na kuimarisha uchumi.

FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI

Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi kwa njia hii zimepuuzwa na viongozi na wafadhili.
Kuku huleta faida kwa jamii kama tulivyoona katika sehemu ya I. Zaidi ya hayo, ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.
· Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
· Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
· Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.

Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:

• Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
• Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai (gharama);
• Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wa kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama)
Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.
Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.
Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku
akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la
kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga
walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wanne
wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudu
nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze
kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.
Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka
iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo
cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje
huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi
nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.
Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo,
huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa
nafaka.
Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku
wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku.
Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.
Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza
kuelezwa hivi:
• Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga
wanne huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza
kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.
Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa
hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo.

TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA

Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya
magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko
kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa
yafuatayo:

Ugonjwa wa Newcastle

Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu
huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida
ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate. Kinyesi chaweza kuwa
na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata
katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa
muda. Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani
aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye
mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.

Minyoo

Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni
piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1
kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au
dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.

Wadudu

Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri
husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii
hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa
mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku
150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa
chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.
Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha
kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.

Magonjwa ya mapafu

Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya
kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa
wingi. Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa.
Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha
kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana
na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati
mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili
vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.
…………………………….//………………………….

KWA UFUPI (SUMMARY)

Kabila za Kuku

Si rahisi kupata kabila halisi (pure breed) au kizazi halisi (pure line) za kuku wa kienyeji kutokana na mwingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Lakini hata hivyo baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kutokana na maumbile yao kwa mfano

1. Kuchi

Warefuna wenye kusimama mgongo ukiwa wima
Wana manyoya machache mwilini na vilemba vyao ni vidogo
Majogoo huwa na wastani wa kilo 2.5 na mitetea kilo 1.8
Mayai gram 45

2. Ching'wekwe (Umbo dogo)

Hupatikana zaidi Morogoro na umasaini
Majogoo kilo 1.6
Mitetea kilo 1.2
Yai gram 37
kuku hawa wanafaa sana kwa biashara ya mayai kwa kuwa hutaga mayai mengi sana.

3. Umbo la Kati

Majogoo kilo 1.9
Mitetea kilo 1.1
Mayai gramu 43
Hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle)

4. Singamagazi

Hupatikana zaidi Tabora
Majogoo wana rangi ya moto na mitetea rangi ya nyuki
Majogoo kilo 2.9
Mitetea kilo 2
Mayai gramu 56

5. Mbeya

Wanapatikana Ileje Mbeya na asili yao ni Malawi
Mjogoo kilo 3
Mitetea kilo 2
Mayai gramu 49
Uwezo wao wa kuatamia mayai na kuangua ni mdogo sana ukilinganisha na kuku wengine

6. Pemba

Maumbo ya wastani na miili myembamba
majogoo kilo 1.5
mitetea kilo 1
mayai gramu 42

7. Unguja

Hawatofautiani sana na wa Pemba
Vilemba vyake ni mchanganyiko- vidogo an vikubwa
Majogoo kilo 1.6
Mitetea kilo 1.2
Mayai gramu 42

SIFA ZA KUKU WA KIENYEJI

Wastahimilivu wa Magonjwa
Wana uwezo wa kujitafutia chakula
Huatamia, kutotoa na kulea vifaranga
Wanastahimili mazingira magumu(ukame, baridi n.k)
Nyama yake ina ladha nzuri

KATIKA KUWAENDELEZA KUKU WA KIENYEJI NI VYEMA

Wajengewe nyumba bora
Wapewe kinga dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle), Ndui (Fowl Pox) pamoja na kinga ya minyoo.
Malezi bora ya vifaranga
Kuwapatia chakula cha ziada pamoja na maji ya kunywa ya kutosha.

NYUMBA BORA

Eneo inapojengwa nyumba au banda la kuku liwe
Linafikika kwa urahisi
Limeinuka juu pasituame maji
Pasiwe na pepo zinazovuma
Vifaa kama miti, nyasi, makuti, fito, udongo mabanzi ya miti, cement, mabati n.k
Sifa za Nyumba Bora ya Kuku
Paa imara lisilovuja
Kuta zisiwe na nyufa
Sakafu isiwe na nyufa
Madirisha ya kutosha kupitisha hewa
Iwe na mlango wa kuingia kufanya usafi
Iwe na ukubwa (nafasi) unaolingana na idadi ya kuku. Wastani wa kuku 10-15 kwa mita moja mraba
Mambo muhimu ndani ya nyumba
Chaga za kulalia kuku
Sakafu iwekwe maranda (wood shavings), makapi ya mpunga, n.k
Viota vya kutagia mayai sentimita 35x35x35 na idadi ya viota iwe nusu ya idadi ya kuku waliofikia hatua ya kutaga na viwekwe sehemu iliyojificha (faragha)

UATAMIAJI WA MAYAI

Kuna njia 2
Njia ya kubuni (incubators)
Asili
Kumuandaa kuku anayeatamia
Weka maranda au majani makavu ndani ya kiota
Anapokaribia kuatamia toa mayai ndani ya kiota pamoja na maranda, hakikisha mikono haina manukato
Nyunyiza dawa ya kuua wadudu (viroboto, utitiri n.k) ndani ya kiota, pia mnyunyizie dawa kuku anayetarajia kulalia mayai
Rudisha mayai kwenye kiota ili kuku aanze kuatamia
Kwa kawaida kuku hulalia mayai yake kwa muda wa siku 21 ndipo huanguliwa

ULEAJI WA VIFARANGA

Kuna njia mbili
Njia ya kubuni
Njia ya asili
Njia ya ASILI
Kuku mwenyewe hutembea na vifaranga akivisaidia kutafuta chakula. Ni vizuri kumtenga kuku mwenye vifaranga katika chumba chake pekee ili vifaranga wasishambuliwe na kuku wengine hali kadhalika kuwalinda na wanyama na ndege wanaoshambulia vifaranga.

Njia ya KUBUNI

Vifaranga huwekwa kwa pamoja kwenye chumba maalum na kupatiwa joto maalum, chakula pamoja na maji. Tumia taa ya kandili (chemli), umeme au jiko la mkaa na hiyo taa iweke kwenye mzingo(mduara) walipo vifaranga. Pia kuna kifaa kinaitwa Kinondoni Brooder ni kizuri kwa kutunzia vifaranga. Kwa kutumia kifaa hiki kuku wanaweza kunyang'anywa vifaranga vyao mara tu baada ya kutotoa na kuviweka kwenye hii brooder na hao kuku wakaachwa bila vifaranga vyao, baada ya majuma matatu au manne, kuku hao huanza tena utagaji na kuendelea na uatamiaji hadi kutotoa tena. Kwa mtindo huu kuku anaweza kutotoa mara 5-6 badala ya kama ilivyo sasa mara 2-3 kwa mwaka. Vifaranga vikae ndani ya brooder majuma 3-4 na baadaye fungua milango ya brooder kuruhusu vifaranga vitoke na kuzungukazunguka chumbani bila kuvitoa nje kw kipindi cha mwezi mmoja au zaidi kutegemeana na mazingira.

KULISHA KUKU WA KIENYEJI

Kuku mkubwa huhitaji gramu 120 za chakula kwa siku, ni vizuri kuku wanaofugwa huria (free range) kupatiwa chakula cha ziada gramu 30 kila siku nyakati za jioni.
Kuku walishwe
Mizizi-mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi, n.k
Nafaka-mahindi, Mpunga, Mtama, Ulezi na Pumba za nafaka zote
Mboga-Mikundekunde, nyanya, milonge, majani ya mapapai
Matunda-Mapapai, maembe, n.k
Mbegu za Mafuta-Karanga, ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, n.k
Unga wa dagaa
Maji

KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU

Pumba………….kilo20
Mashudu ya Pamba n.k…kilo 3
Dagaa iliyosagwa………kilo 1
Unga wa majani uliokaushwa kivulini na kusagwa……..kilo 2
Unga wa Mifupa ……….kilo 0.25
Chokaa ya mifugo ……..kilo 0.25
Chumvi……………………gramu 30
Vichanganyio/Premix…gramu 25

KUPANDISHA

Uwiano wa mitetea na jogoo ni mitetea 10-12 kwa jogoo mmoja
Sifa za mtetea ni mkubwa kiumbo, mtagaji mayai mengi, muatamiaji mzuri na mlezi wa vifaranga
Sifa za jogoo ni awe mkubwa kiumbo, miguru imara na yenye nguvu, mrefu, upanga/kilemba kikubwa, awe na uwezo wa kuitia chakula mitetea na awe na tabia ya kupenda vifaranga
Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10 na kuendelea hadi miaka mitatu na asipande watoto wake
Mitetea huanza kutaga wakiwa na miezi 6-8

MAGONJWA YA KUKU

1. Mdondo/New castle
Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa

Dalili

Kuhalisha choo cha kijani na njano
Kukohoa na kupumua kwa shida
Kupinda shingo kwa nyuma
Kuficha kichwa katikati ya miguu
Kukosa hamu ya kula na kunywa
Idadi kubwa ya vifo hadi 90%

Kinga

Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
Epuka kuingiza kuku wageni
Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
Zingatia usafi wa mazingira

NDUIYA KUKU/ FOWL POX

Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu

Dalili

Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana
Kukosa hamu ya kula
Vifo vingi

Kinga

Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
Epuka kuingiza kuku wageni
Zingatia usafi wa mazingira

HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID

Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
Kuku hukosa hamu ya kula
Kuku hukonda
Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
Kinyeshi hushikamana na manyoya

Tiba

Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga

Usafi

Fukia mizoga
Usiingize kuku wageni
Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6

MAFUA YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA

Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku wakubwa

Dalili

Kuvimba uso
Kamasizilizochanganyikana na usaha unaonuka
Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
Hukosa hamu ya kula
Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya
Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamini

KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS

Husababishwa na vijidudu vya Protozoa

Dalili

Kuharisha damu
Manyoya husimama
Hulala na kukosa hamu ya kula

MINYOO

Dalili

Kunya minyoo
Hukosa hamu ya kula
Hukonda au kudumaa
Wakati mwingine hukohoa
Tiba
Dawa ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu

WADUDU

Viroboto, chawa, utitiri

Dalili

Kujikuna na kujikung'uta
Manyoya kuwa hafifu
Rangi ya upanga kuwa hafifu
Ngozi kuwa nene, ngumu na yenye magamba yanayodondoka kama unga
Kuzuia
Ziba mipasuko sakafuni na kwenye kuta za banda
Fagia banda mara mbili kwa wiki
Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
Nyunyiza dawa kwenye viota
Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
Fuata kanuni za chanjo
Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima

UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA

Dalili

Kuku hupungua damu, uzito na kudumaa
Mifupa huwa laini na kutokuwa imara
Hutaga mayai yenye gamba laini na madogo
Huwa na manyoya dhaifu

ufugaji wa nguruwe

Nguruwe ni mnyama mwenye faida, ni rafiki kwa mazingira na hahitaji gharama kubwa

“Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa kisasa ili kupata mazao bora. Unaweza kupata kila unachohitaji wewe, familia na hata ndugu zako kutokana na ufugaji wa nguruwe”, anasema Bwana Lomaiyani Molel kutoka Arusha. Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo.

Ufugaji


Kwa kawaida nguruwe wanafugwa na watu wa kada zote, wafugaji wadogo wadogo na hata wakubwa. Aina hii ya ufugaji huweza kumpatia mkulima kipato pamoja na lishe kwa familia, na hauhitaji gharama kubwa.


Banda


Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa vifaa nafuu. Unaweza kutumia mchanga na simenti kuweka sakafu, ama ukatumia udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kuweka sakafu. Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.


Malisho


Ulishaji wa nguruwe ni rahisi kwa kuwa wanakula aina mbalimbali za vyakula kulingana na mazingira wanayofugwa. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali, na pia hulishwa kwa kutumia masalia ya nafaka (pumba). Unaweza kuwalisha kwa kutumia mashudu au pumba aina ya Wheat Poland. Pia unaweza kuwalisha kwa kutumia mabaki ya jikoni.


Kuzaliana


Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 8 wanakuwa na uzito kati ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa.


Matunzo


Baada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.


Magonjwa yanayoathiri nguruwe


Kuna aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini yapo yale yaliyozoeleka ambapo ni lazima kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji wenye tija.


Ugonjwa wa miguu na midomo


Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.


Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja. Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo.


Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.


Homa ya Nguruwe (Swine fever)


Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa homa ya nguruwe huenea kwa haraka sana miongoni mwa makundi ya nguruwe, na huua kwa haraka sana, lakini hauna madhara kwa binadamu na hauambukizwi kwa binadamu. Nguruwe walioambukizwa waanshikwa na vindonda ama mapunye kwenye ngozi. Pia masikio na ngozi huwa mekundu.


Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.


Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine.


Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia)


Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.


Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.


Kimeta (Anthrax)


Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi.


Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.


Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.


Muhimu: Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.


Ushauri: Kwa ushauri zaidi juu ya ufugaji wa Nguruwe na magonjwa ya wanyama, unaweza kuwasiliana na Mtaalamu wa mifugo Bwana Oletikoishi Wawaa, simu 0754 207 987.

Itikio 97 kwa “Ufugaji wa nguruwe ni rahisi na wenye tija”



Njia rahisi za upatikanaji wa vifaranga wengi



Kuna njia tofauti za kuanza au kuongeza mtaji kwa mfugaji wa kuku kama vile, kununua kuku wakubwa, vifaranga kutoka kwa wafugaji wengine au kuzalisha vifaranga wako wewe mwenyewe.

Copy of IMG_0444 2
Ni muhimu kuku kupata sehemu ya wazi wanayoweza kutembea
Kwa wafugaji wengi ambao wana lengo la kufuga kuku wengi wa umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.


Kwa nini kuwa na vifaranga wengi wa umri mmoja?

Kupunguza gharama za ufugaji kwa mfano chanjo na tiba;
  • Kutunza kuku kitaalam kwa urahisi
  • Kupata mayai mengi kwa wakati mmoja
  • Kuuza kuku wengi kwa waakti mmoja
  • Kuwapa uhakika wateja wako


Hivyo kuna njia kuu mbili za upatikanaji wa vifaranga wengi kwa wakati mmoja nazo ni;
  1. Kwa kuhatamiza kuku wengi kwa wakati mmoja
  2. Kwa njia ya mashine ya kuangulia incubator)
  3. Njia zote mbili huweza kutoa vifaranga bora bali uchaguzi wa njia ipi itumike utatokana na mtaji wa mfugaji na mahali alipo.


Kwa kuhatamiza kuku wenyewe


Njia hii hutumika kuhatamisha tetea wengi kwa wakati mmoja hivyo mfugaji anatakiwa achague mitetea, mayai, aandae viota, maji na chakula bora.


Sifa za tetea wa kuhatamia
  • Kuku mwenye umbo kubwa
  • Mwenye uwezo na historia nzuri ya kuhatamia na hatimaye kutotoa vifaranga

Sifa za mayai ya kuhatamisha
  • Mayai ya siku ya mwisho kutagwa ndio yawe ya kwanza kuwekwa yafuatiwe na ya siku zinazofuata yasizidi wiki mbili tangu kutagwa
  • Lisiwe kubwa sana au la duara, lisiwe na uvimbe
  • Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa


Sifa za kiota na chumba cha kuhatamia
  • Kuku wanaohatamia watengwe katika chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana.
  • Mlango na dirisha viwekwe wavu ili muda wa mchana mwanga na hewa uweze kuingia ndani.
  • Chumba kiwe na nafasi ya kutosha kuweka viota, chakula na maji.
  • Ili kutumia eneo vizuri viota vinaweza kutengenezwa ukutani kama mashelfu.
  • Viota viundwe vizuri kwa nyasi, maranda makavu ya mbao, au nguo ya pamba lakini isiyo tetroni.
  • Viota visiwe sehemu yenye unyevunyevu.
  • Idadi ya viota vilingane na idadi ya matetea walio chaguliwa kuatamia
  • Vinyunyiziwe dawa ya kuuwa wadudu kama utitiri kwani hawa ni wadudu wasumbufu ambao husababaisha kuku kutokatoka nje, hivyo kupunguza uwezekano wa mayai kuanguliwa yote.


Copy of chickensChakula, vitamini na maji

Kuku wanaohatamia wapewe chakula cha kuku wakubwa wanaotaga (layers mash) cha kutosha muda wote kiwemo kwa kua kuku hawa hutoka wakati tofauti pia majani, mboga-mboga na maji ya kunywa ni muhimu sana. Vyote hivi viwekwe kwenye chumba ambacho kuku wanahatamia ili kumfanya kuku asiende umbali mrefu kutafuta chakula pia kuyaacha mayai kwa muda mrefu.


Hatua za kuhatamisha kuku
  1. Kuandaa viota, uchaguzi wa matetea bora na kuandaa mayai.
  2. Tetea wa kwanza akianza kuhatamia muweke mayai yasio na mbegu ama viza.
  3. Rudia zoezi hili mpaka itakapo fikia idadi ya kuku unao wahitaji.
  4. Baada ya kupata idadi ya kuku wawekee mayai yenye mbegu.

N.B. kuku wote waliochaguliwa kwa ajili ya kuhatamia wawekwe wakati wa usiku kwa sababu ya utulivu uliopo.


Kwa kupitia njia hii kuku mmoja anaweza kuhatamia hadi mayai 20 ukizingatia sifa za kuku huyo. Baada ya kutotoa hatua ya awali ya uleaji wa vifaranga. Kuku wazazi hutengwa na vifaranga ambapo vifaranga hupewa joto na mwanga kwa kutumia taa ya umeme, jiko au kandili. Maji yenye glucose kwa ajili yakuongeza nguvu, pia chakula.


Changamoto
  • Huhitaji sehemu kubwa kwa sababu ili upate vifaranga wengi unahitaji kuku wengi wanao atamia.
  • Kuwepo kwa wadudu kama utiriri na kutopatikana kwa chakula cha kutosha husababisha kuku kutoka toka nje na kusababisha mayai kuharibika.
  • Kuku kupata magonjwa wakati wanapo atamia.
  • Kutokuwa na kipimo cha kupimia mayai yaliyo na mbegu


Ushauri kutoka kwa mfugaji: Wakulima tubadilike na kuanza kufuga kibiashara kwa kua soko la mazao ya kuku wakienyeji lipo. Pia tuweze kuzalisha mayai bora ya kutotolesha, ni muhimu sana yatokane na kuku wako ama kwa mfugaji ambaye una uhakika na ufugaji wake.


Itikio 44 kwa “Njia rahisi za upatikanaji wa vifaranga wengi”

UZALISHAJI BORA WA MAZIWA KWA BEI NAFUU

 

Lishe bora: Ng’ombe hawezi kulaumiwa kwa kushindwa kufanya urutubishaji. Ukosefu wa lishe sahihi husababisha ng’ombe kuwa dhaifu na pia husababisha kutokea kwa magonjwa ambayo huweza kuathiri mfumo wa uzazi.


resheni
Malighafi zinazotumika kutengeneza chakula cha mifugo nyumbani
Kupungua kwa ulaji wa vyakula vya kutia nguvu huathiri joto na hatimae kupunguza uwezo wa uzalishaji kwa ng’ombe. Hii ina maana, lishe hafifu kwa ng’ombe wa maziwa husababisha ng’ombe kutokupata joto kwa wakati uliotarajiwa kwa sababu miili yao haipo katika hali nzuri ya kubeba mimba. Ng’ombe lazima alishwe mlo kamili unaojumuisha wanga, protini, madini na vitamini.


Utafiti unaonesha kwamba ng’ombe aliyeathirika kutokana na utapiamlo, baada ya mwili wake kujijenga kwa upya na kuwa katika hali ya kawaida, huweza kujirudia katika hali ya uzalishaji na akashika mimba kwa haraka sana hata kuliko ng’ombe aliyekuwa akipata mlo kamili kwa wakati wote.


Uzalishaji wa lishe

Ng’ombe anayelishwa nyasi tu hawezi kufikia kiwango kizuri cha uzalishaji maziwa hivyo anahitaji kupatiwa lishe ya ziada. Virutubisho vya ziada kama vile dairy meal inakadiriwa kugharimu asilimia 20% zaidi ya gharama ya jumla ya uzalishaji wa maziwa, hivyo kupunguza faida kwa mfugaji.


Kuongeza virutubisho vinavyochochea uzalishaji wa maziwa kwa kutumia lishe ya asili inayopatikana kwenye mazingira ya mfugaji na yenye gharama nafuu husaidia wafugaji kupata maziwa mengi kwa gharama ya chini. Ili virutubisho vya ziada kuwa na manufaa kwa ng’ombe ni lazima uwepo uwiano wa upatikanaji wa nishati, protini na madini.


Vyanzo vya wanga: Mahindi, makapi ya ngano, molasesi, pumba ya mahindi, na pumba ya ngano.
Vyanzo vya protini: Nyasi, mbegu za pamba, soya, mbegu za alizeti, majani ya sesbania, majani ya kaliandra, na dagaa.
Vyanzo vya madini: Kalishamu, fosifeti, mawe ya chokaa, pamoja na madini ya premix.


Namna ya kuchanganya virutubisho vya uzalishaji wa maziwa


1. Uzalishaji wa kawaida

Kufanya mchanganyiko wa kilo 100;
• Kilo 75 ya lishe ya wanga
• Kilo 23 ya lishe ya protini
• Kilo 2 za madini

Kwa mfano;
• Kilo 57 za mahindi
• Kilo 18 za makapi ya ngano
• Kilo 17 za lusina
• Kilo 6 za soya
• Kilo 2 za fosifeti


2. Uzalishaji wa maziwa kwa kiwango cha juu

Kufanya mchanganyiko wa Kilo 100;
• Kilo 68 za lishe ya wanga
• Kilo 30 za lishe ya protini
• Kilo 2 za lishe ya madini

Kwa mfano;
• Kilo 50 za mahindi
• Kilo 16 za makapi ya ngano
• Kilo 2 za molasesi
• Kilo 14 za mbegu za pamba
• Kilo 12 za lusina
• Kilo 4 za dagaa


Faida za mchanganyiko unaotengenezwa kiasili

• Una ubora sawa na lishe zinazouzwa.
• Gharama yake ni ndogo ukilinganisha na lishe ya kununua.
• Hukubalika kwa ng’ombe.
• Ni rahisi kutunza na kutengeneza.




 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni